Wakati methali ya Kiswahili inasema “haba na haba hujaza kibaba”, Mshauri Mwenezi wa Stadi za Maisha, Siegfried Mbuya, amewakumbusha vijana na jamii kwa ujumla kuwa mafanikio ni safari inayohitaji subira, bidii na hatua za kimkakati, badala ya kutafuta mafanikio ya haraka yasiyo na misingi imara.
Akizungumza katika mahojiano maalumu kwenye kipindi cha #Hellowikiendi, Mbuya amesema kuwa kila mafanikio katika maisha yanaanzia kwenye hatua ndogo na kuongezeka taratibu, hali inayojenga msingi wa kudumu na kuheshimu utamaduni wa kila mmoja.
✍Ibrahim Kilumbo
Mhariri | @claud_jm
#azamtvupdates😂😂😂😂😂