
China imetangaza leo Jumatatu, Desemba 29, mazoezi makubwa ya kijeshi kuzunguka Taiwan, ikiwa ni pamoja na mazoezi ya kurusha makomora na risasi za moto yaliyopangwa kufanyika Desemba 30 katika maeneo matano ya majini na angani karibu na kisiwa hicho.
Imechapishwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
“Kuanzia Desemba 29, Kamandi ya Mashariki ya PLA (jeshi la China) itapeleka wanajeshi wake wa Jeshi nchi kavu, Jeshi la Wanamaji, Jeshi la Anga, na Kikosi cha Makombora kufanya mazoezi ya pamoja ya kijeshi yaliyopewa jina la Mission Justice 2025,” kulingana na taarifa kutoka kwa Kanali Shi Yi, msemaji wa Kamandi.
“Kwa sababu za kiusalama, meli na ndege zote ambazo hazihusiki zinashauriwa kutoingia katika maeneo ya majini na angani yaliyotajwa hapo juu,” taarifa hiyo imesema. Onyesho hili kubwa la nguvu linakuja baada ya wiki kadhaa za mvutano kati ya China na Japan, ambalo lilianza na taarifa zinazopendekeza kwamba Tokyo inaweza kuiunga mkono Taiwan iwapo kutatokea mzozo wa kijeshi katika siku zijazo.
Hii pia inafuatia mauzo ya hivi karibuni ya silaha ya Marekani kwa Taipei, ambayo yameikasirisha Beijing, ambayo ilijibu wiki iliyopita kwa kuweka vikwazo kwa makampuni 20 ya ulinzi ya Marekani. Taiwan, kwa upande wake, inalaani “vitisho vya kijeshi” vya Beijing.