
Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje wa China Lin Jian bila ya kutaja taifa lolote aidha Taiwan kijeshi na kusema hatua hiyo inauingiza Mlango wa Bahari wa Taiwan katika hatari ya vita.
Hatua hiyo imesababisha serikali mjini Taipei kulaani kile ilichotaja “vitisho vya kijeshi” vya Beijing.
Amesema “Nataka kusisitiza kuwa dhamira ya China katika kulinda uhuru wa kitaifa, usalama na uadilifu wa eneo lake la mipaka haitoyumba. Vitendo vyovyote vinavyosababisha uchochezi na kuvuka mipaka katika suala la Taiwan vitajibiwa vikali na China.”
Hatua hii ni baada ya Marekani, ambayo ni mshirika mkubwa wa Taiwan kuiuzia kiwango kikubwa cha silaha.