WAZIRI Mkuu, Dk. Mwigulu Nchemba, leo Desemba 29, 2025, amefanya ukaguzi wa uzalishaji na usambazaji wa maji katika eneo la Ruvu Chini, mkoani Pwani. Ukaguzi huu ni sehemu ya jitihada za Serikali kuhakikisha wananchi wanapata maji safi na ya kutosha.

Akizungumza baada ya ukaguzi, Dk. Mwigulu amesema Serikali imeanza kutekeleza miradi mbalimbali ya maji katika kipindi cha miaka mitatu iliyopita ili kukabiliana na upungufu wa maji unaosababishwa na mabadiliko ya tabia ya nchi. SOMA: Dk Mwigulu akagua maendeleo ujenzi madaraja Lindi

Amesema miradi hiyo mikubwa inalenga kutoa matokeo chanya kwa wananchi wa Pwani. “Mipango hii ya ujenzi wa miradi ilianza muda mrefu. Serikali iliona changamoto ya upungufu wa maji na kuanza kutafuta majawabu miaka mitatu iliyopita kwa kujenga miradi mikubwa itakayosaidia kutoa maji kwa wananchi,” alisema Dk. Mwigulu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *