Watu sita, akiwemo msichana wa miaka miwili, wameuawa siku ya Jumapili, Desemba 28, karibu na ufuo wa watalii kusini-magharibi mwa Ecuador wakati wa shambulio la bunduki ambalo pia lilisababisha watu wengine watatu kujeruhiwa, polisi imetangaza.

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Tukio hilo lilitokea Puerto Lopez, katika jimbo la Manabi, eneo maarufu wanakotazama nyangumi, huku kukiwa na wimbi la vurugu mwishoni mwa wiki hii iliyopita zilizogharimu maisha ya watu tisa katika jiji hilo, kulingana na vyombo vya habari vya ndani.

Wakati wa shambulio katika eneo hili la Puerto Lopez, “watu sita waliuawa na wengine watatu walijeruhiwa,” Kanali William Acurio, kamanda wa polisi wa eneo hilo, amewaambia waandishi wa habari siku ya Jumapili. Miongoni mwa waliofariki alikuwa msichana “mwenye umri wa kama miaka miwili,” ameongeza.

Ecuador, iliyoko kati ya wauzaji wawili wakuu wa kokeini duniani, Colombia na Peru, imeshuhudia kuibuka tena kwa vurugu kutokana na mapigano kati ya magenge ya wahalifu yanayohusiana na magenge ya Mexico na Colombia.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *