Kura zinaendelea kuhesabiwa nchini Guinea, kufuatia uchaguzi mkuu uliofanyika hapo jana, uchaguzi ambao kiongozi wa kijeshi, Mamady Doumbouya anatarajiwa kushinda.
Imechapishwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Uchaguzi wa Jumapili ya wiki iliopita ulifanyika bila ya ushiriki wa wapinzani wakuu akiwemo Cellou Diallo, ambaye alizuiwa kushiriki wakati huu akiwa uhamishoni.
Kwa sehemu kubwa zoezi la upigaji kura lilifanyika katika mazingira ya amani bila ya ripoti zozote za kuwepo vurugu, ingawa kuelekea zoezi hilo waangalizi wa kimataifa ikiwemo umoja wa Mataifa walionya kuhusu kukosekana kwa usawa na pia vitisho dhidi ya wapiga kura.

Doumbouya aliingia madarakani mwaka 2021 baada ya mapinduzi ya kijeshi ambapo licha ya kuahidi kurejesha utawala wa kiraia, alijitangaza kuwa mgombea huru, huku kwa muda wa miaka minne amekuwa akiwabana wakosoaji wake kwa kuwafunga na wengine kulazimika kukimbia nchi yao.
Juma ya wapiga kura milioni 6 na laki 8 walijiandikisha kupiga kura, hata hivyo kumeshuhudiwa idadi ndogo ya watu waliojitokeza ambapo wizara ya mambo ndani ikitarajiwa kutangaza matokeo ya awali kuanzia hapo kesho.
Doumbouya alikuwa akishindana na wagombea wengine 8 ambao hawana umaarufu wa kisiasa.