#HABARI: Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, SACP Alex Mkama, amefanya ziara ya kikazi katika eneo la Iyovi, wilayani Kilosa, kukagua hali ya usalama baada ya kifusi cha matope kuporomoka na kuziba barabara kuu ya Morogoro-Iringa. Changamoto hiyo imetokana na mvua kubwa zinazoendelea kunyesha mkoani humo, hali iliyosababisha kukwama kwa mawasiliano ya barabara na kuhatarisha usalama wa wasafiri na watumiaji wengine wa njia hiyo muhimu.
Akiwa katika eneo la tukio, Kamanda Mkama ametoa rai kwa madereva na wananchi wanaotumia barabara hiyo kuwa waangalifu na kuzingatia alama za usalama wakati huu wa dharura za kimaumbile. Amesisitiza umuhimu wa kuchukua tahadhari kubwa ili kuepusha ajali na madhara yanayoweza kujitokeza, huku juhudi za kuondoa kifusi hicho na kurejesha hali ya kawaida zikiendelea kwa ushirikiano wa mamlaka husika.
Powered by #MCHEZOSUPA
JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:
–
Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.
#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania