Halmashauri ya Jiji la Dodoma imetoa notisi ya siku 21 kwa waombaji wa viwanja katika maeneo ya Mtumba na Kikombo waliochelewa kukamilisha mchakato wa malipo ndani ya muda uliopangwa, ikiwataka kulipia viwanja hivyo kabla ya kutaifishwa na kuuzwa upya.

Kwa mujibu wa halmashauri hiyo, jumla ya viwanja 6,560 vimevuka muda wa malipo na kusababisha upotevu wa zaidi ya shilingi bilioni 55.4 za mapato ya ndani, hali inayokwamisha utekelezaji wa miradi ya maendeleo na mipango ya uendelezaji wa jiji.

✍George Mbara
Mhariri | @claud_jm

#AzamTVUpdates

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *