Harakati za vyama vya wafa­nyakazi Tanzania zimepitia katika vipindi tofauti vya kisiasa na kiu­chumi. Harakati hizo ziliendesh­wa wakati wa ukoloni na baada ya uhuru. Kabla ya uhuru (Wakati wa Ukoloni) vyama vya wafanyakazi viliendeshwa kwa uhuru na usawa lakini baada ya uhuru vilikuwa seh­emu ya chama tawala.

Kwa mfano, kati ya mwaka 1964 na 1978 NUTA ilikuwa ni sehemu ya Tanganyika African National Union (TANU). Pia kati ya miaka ya 1978 hadi 1991 Jumuiya ya Wafa­nyakazi Tanzania (JUWATA) ili­kuwa ni moja ya Jumuiya muhimu ya Chama cha Mapinduzi (CCM). Tofauti hizi hazikuathiri tu miun­do ya vyama vya wafanyakazi laki­ni pia zilichangia kubadili tabia na mitizamo yake.

Chama cha Wafanyakazi wa Viwanda, Biashara, Taasisi za Fed­ha, Huduma na Ushauri (TUICO) ni chama cha pekee cha wafanya­kazi hapa Tanzania kinachohu­dumia wafanyakazi kutoka taasisi za umma na binafsi na kinaundwa na sekta nne ambazo ni viwanda, biashara, taasisi za fedha, huduma na ushauri.

Vyama vya wafanyakazi vime­kuwa vikisukumwa na matukio mbalimbali yanayotokana na mabadiliko katika mifumo ya kijamii na kiuchumi, aidha mabadi­liko ya kiuchumi yaliyoikumba nchi miaka ya 90 pia yalibadili mfumo wa Vyama vya Wafanyakazi.

TUICO kilianzishwa mwaka 1995 pamoja na vyama vingine 10 na kujishirikisha katika Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi Tanzania Federation of Free Trade Union (T­FTU) mwaka 1998 na baadae TUC­TA (Trade Union Congress of Tan­zania) mwaka 2001.

Kwa takribani miongo mitatu, TUICO si tu kimekuwa mstari wa mbele katika kutetea haki za wafa­nyakazi, bali pia kimekuwa kiun­ganishi cha mahitaji ya uchumi unaobadilika na kulinda heshima na ustawi wa wafanyakazi.

Kama inavyofahamika kuwa, uchumi wa Tanzania umepitia mabadiliko makubwa tangu miaka ya 1990 ubinafsishaji, uwekezaji wa kigeni, uanuwai wa viwanda na kuibuka kwa huduma za kidijitali. Ingawa haya yameongeza ajira, pia yameleta changamoto, usalama wa ajira umepungua, mikataba ya muda mfupi imeenea, na wafanya­kazi wengi wamejikuta wakifanya kazi katika mazingira yasiyo rasmi au yenye maslahi duni.

Katika muktadha huu wa maba­diliko, TUICO imeendelea kuwa thabiti katika kukabiliana na chan­gamoto hizo. Kupitia majadiliano ya pamoja na mikataba ya hali bora (CBAs) ili kuboresha mishahara, kuhakikisha haki, na kuimarisha ulinzi wa maslahi kwa maelfu ya wafanyakazi. Mikataba hii iliyop­kina na waajiri imeleta maba­diliko chanya katika maisha ya wafanyakazi wengi nchini.

Kwa TUICO, harakati hizi si suala la mishahara pekee ni jitihada za kulinda na kubore­sha utu na hadhi ya mfanyakazi katika dunia ya ajira. Tukiwa na mtazamo kuwa wafanyakazi si mshirika muhimu wa maende­leo ya Tanzania, bali ni injini ya maendeleo inayostahili usalama, maisha ya heshima, na sauti kati­ka kuamua mustakabali wao.

Ustawi na usawa wa kijinsia

Mbali na kulinda masilahi ya wafanyakazi, juhudi za chama hazijaishia kwenye majadiliano ya mishahara pekee. Kimeen­delea kusimamia pia ajenda ya kujenga mazingira ya kazi yenye haki ikizingatia ustawi na usa­wa wa kijinsia kwa mapana yake, kupitia kushinikiza upatikanaji wa bima ya afya kwa wafanya­kazi na wategemezi wao, posho za makazi, posho za usafiri na mafao ya pensheni chini ya mfu­mo wa hifadhi ya jamii wa Tan­zania.

Katika mapambano yetu ya kila siku, tumejitolea kuendele­za usawa wa kijinsia katika seh­emu za kazi. Katika sekta kama benki, huduma za wageni, na biashara za rejareja ambazo zina wafanyakazi wengi wanawake, tumeendelea kusimamia malipo sawa kwa kazi sawa, ulinzi dhidi ya unyanyasaji kazini na kuhaki­kisha wanawake wanawakil­ishwa ipasavyo katika nafasi za uongozi, si tu katika maeneo ya kazi bali pia ndani ya chama che­tu.

Pia kupitia programu zetu za kujenga uwezo, tumewawezesha wanawake kushiriki kikamilifu katika majadiliano na mchakato wa kufanya maamuzi. Kwa njia hii, tunapambana na tofauti za kijinsia ambazo bado zinaathi­ri sekta nyingi, na tunajenga mazingira ya haki na usawa kwa kila mfanyakazi.

Kipaumbele kwa usalama kazini

TUICO imejizatiti kuvisimamia ni kuhakikisha usalama na afya mahali pa kazi. Kwa kushiriki­ana na Mamlaka ya Usalama na Afya Mahali pa Kazi (OSHA) na wadau wengine, tumekuwa mstari wa mbele katika kuhaki­kisha kwamba wafanyakazi wan­apewa mafunzo, vifaa na uelewa wa kutosha ili kudai mazingira salama ya kazi.

Katika viwanda, maghala, na biashara mbalimbali, tumeende­lea kutetea utekelezwaji wa she­ria za usalama za kitaifa, kuhimi­za ukaguzi wa mara kwa mara wa sehemu za kazi, na kushinikiza upatikanaji wa vifaa kinga kwa wafanyakazi. Juhudi zetu zisi­zochoka zimechangia kupungua kwa ajali na vifo kazini, na hivyo kuthibitisha kuwa kulinda mai­sha ya wafanyakazi si jambo lina­lowezekana tu, bali ni la lazima.

Pamoja na hayo, tunashirik­iana kwa karibu na Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF) ili kuhakikisha kuwa wale wana­oumia au kuathirika kiafya kuto­kana na kazi zao wanapata fidia stahiki kwa wakati muafaka

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *