Leo ni Jumatatu 8 Rajab 1447 Hijria mwafaka na 29 Disemba 2025.
Siku kama ya leo mwezi 8 Rajab, yaani miaka 414 iliyopita kwa mujibu wa kalenda na Hijria, alizaliwa faqihi na mwanazuoni mashuhuri wa Kiislamu Sheikh Abu Jaafar Muhammad bin Hassan maarufu kwa jina la Sheikh Hurr al Aamili huko Jabal Amil nchini Lebanon.
Baada ya utafiti na uchunguzi wa muda mrefu Sheikh Aamili alitokea kuwa miongoni mwa maulama wakubwa wa zama hizo hususan katika elimu za fiqhi na Hadithi.
Sheikh Hurr al Amili ameandika vitabu vingi katika taaluma hizo kikiwemo kile cha Wasailu Shia ambacho kina nafasi maalumu katika elimu ya fiqhi. Kitabu kingine muhimu cha mwanazuoni huyo ni Hidayatul Ummah. Mwanazuoni huyo aliaga dunia mwaka 1114 Hijria.

Siku kama ya leo miaka 119 iliyopita, katiba ya Iran ya ufalme wa kikatiba iliyoandikwa na Bunge la kwanza la taifa ilitiwa saini na kupasishwa na mfalme wa wakati huo wa Iran, Mozaffaruddin Shah Qajar.
Katiba hiyo ilikuwa na vipengee 51 ambavyo baadaye viliongezwa vifungu 107 kama vikamilisho. Katika kipindi cha miaka iliyofuata na katika zama za tawala mbalimbali hususan katika kipindi cha utawala wa kidikteta wa Kipahlavi, katiba hiyo ilifanyiwa marekebisho ya kimsingi. Akthari ya marekebisho hayo yalikuwa na madhara ya mamlaka ya wananchi na Uislamu.

Miaka 95 iliyopita katika siku kama ya leo aliaga dunia Theodor Nöldeke msomi wa Kijerumani na mtaalamu wa mambo ya nchi za mashariki.
Alihitimu masomo yake katika taaluma ya teolojia, falsafa pamoja na lugha mbalimbali na kutunukiwa shahada ya uzamivu. Theodor Nöldeke alianza kufundisha Chuo Kikuu akiwa na umri wa miaka 25 na kuifanya kazi hiyo kwa miaka mingi.
Theodor Nöldeke alikuwa amebobea katika lugha za Kiarabu, KIifarsi, Kituruuki, Kigiriki, Kihispania na Kitaliano.

Katika siku kama ya leo miaka 88 iliyopita, mkataba wa kupata uhuru Jamhuri ya Ireland ulitiwa saini baina ya viongozi wa wapigania jamhuri wa Ireland na utawala wa wakati huo wa Uingereza.
Hata hivyo kutokana na kuanza Vita vya Pili vya Dunia, serikali ya Uingereza ilikataa kutekeleza mkataba huo. Baada ya vita hivyo, mnamo mwaka 1949, Jamhuri ya Ireland ya Kusini ilijitangazia rasmi uhuru wake toka kwa mkoloni Muingereza.
Uhuru wa Ireland ulikuwa matokeo ya mapambano ya karne nane ya wapigania Jamhuri wa Ireland dhidi ya Uingereza.

Siku kama ya leo miaka 3 iliyopita, Pele gwiji mashuhuri wa soka aliaga dunia.
Edson Arantes do Nascimento anayejulikana kama Pele, alizaliwa mnamo Oktoba 23, 1940 huko Tinejos, Brazil. Pele ambaye anajulikana kama mmoja wa wachezaji bora wa soka katika historia, alikulia katika familia maskini na alikuwa akipenda sana mpira wa miguu tangu utoto. Alianza kucheza soka akiwa na umri wa miaka 10 na alijiunga na timu ya Santos akiwa na umri wa miaka 15. Aliitwa katika kikosi cha timu ya taifa ya soka ya Brazil kwa mara ya kwanza akkiwa na umrii wa miaka 17.
Pele alishiriki kombe la dunia mara nne akiwa na timu ya soka ya Brazil. Aidha pele alichezea Brazil mechi 92 na kurfunga mabao 77. Mwaka 2000 Pewle alichaguliwa kuwa mchezaji bora wa karne. Pele a;ishinda mataji 3 ya kombe la dunia akiiwa na timu ya soka ya Brazil katika miaka ya 1958, 1962 na 1970.
