
Rais wa Marekani Donald Trump alisema alifurahishwa kwamba mzozo huo umehitimishwa haraka na kwa njia ya haki,” akiongeza kwamba Washington “inajivunia kusaidia.” Naye Waziri wa Mambo ya Nje wa China Wang Yi aliyaita makubaliano hayo “hatua muhimu kuelekea kurejesha amani,” akiongeza kuwa “yanaendana na matarajio ya pamoja ya nchi za eneo hilo.”
Chini ya mpango huo, pande zote mbili zimetakiwa kusitisha mapigano ya wiki kadhaa katika mpaka wao unaogombaniwa ambayo yamewaua zaidi ya watu 100 na kuwalazimu watu zaidi ya nusu milioni katika nchi zote mbili kuhama makwao. Makubaliabo hayo ya usitishaji mapigano yalionekana kuheshimiwa siku moja baada ya kutiwa saini, huku China, ambayo ilikuwa na jukumu muhimu la upatanishi, ikiandaa mazungumzo na mataifa hayo yanayozozana katika mkoa wa kusini magharibi wa Yunnan. Waziri wa Mambo ya Kigeni wa Thailand Sihasak Phuangketkeow na Waziri wa Mambo ya Nje wa Cambodia Prak Sokhonn walipangiwa kukutana na waziri mwenzao wa China Wang Yi.