Katika taarifa iliyotolewa na mamlaka hiyo, TMA iliorodhesha mikoa hiyo ambayo itaathirika na mvua kubwa kuwa Arusha, Kilimanjaro, Manyara, Kigoma, Katavi, Singida, Dodoma, Rukwa, Songwe na Morogoro.
Mikoa mingine ambayo pia yamewekwa kwenye tahadhari ni Ruvuma, Tanga, Dar es Salaam, Pwani ikiwemo Kisiwa cha Mafia, Lindi, Mtwara, pamoja na visiwa vya Unguja na Pemba. Mamlaka ya Hali ya Hewa inasema mvua kubwa inaweza kuleta athari mbalimbali.
Miongoni mwa athari zinazotabiriwa ni mafuriko, maporomoko na kutatiza shughuli za uchumi na za kijamii za watu.