Mvua kubwa zinazoendelea kunyesha katika maeneo mbalimbali mkoani Tabora zimeleta adha kwa wananchi wa kata ya mapambano na kijiji cha masagala vilivyopo manispaa ya Tabora baada ya bwawa la Italia kufurika maji na kisha kuvunja tuta la kingo za bwawa hilo na hivyo kusababiasha wanchi kukosa mawasiliano ya uhakika baada ya kukatika kwa barabara muhimu zinazounganisha maeneo hayo.

Baadhi ya wanachi waliokubwa na adha hiyo ya kukatika kwa mawasiliano ya barabara wanaiomba mamlaka husika kuchukua hatua za makusudi ili kuwanusuru na kadhia hiyo.

✍️ @pendo_salu

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *