
Lin amesema nchi “zilizoko nje ya kanda hiyo zinatakiwa kuacha kuingilia masuala ya huko bila msingi. Nchi yoyote haitakiwi kuunga mkono kujitenga kwa nchi zingine kwa maslahi yao binafsi.”
Msemaji huyo wa wizara ya China pia alitoa wito kwa mamlaka za Somaliland “kutathmini kuhusu muelekeo wao” na mara moja waache suala lolote la kujitenga na “mkwaruzani na watu kutoka nje.”
Siku ya Ijumaa Israel imekuwa nchi ya kwanza duniani kutambuwa Somaliland kama taifa huru, kusababisha kukataliwa kwa hatua hiyo na mataifa kadhaa ya Afrika na Mashariki ya Kati, ikiwemo Uturuki, ambayo ilikuwa sehemu ya taarifa ya Jumamosi iliyotolewa na Qatar.
Somaliland ilijitangazia uhuru kutoka kwa Somalia 1991 na imekuwa taifa linalojitegemea kwa zaidi ya miongo mitatu, lakini halijawahi kutambuliwa rasmi na taifa lolote mwanachama wa Umoja wa Mataifa.
Serikali ya Somalia inakataa kutambuwa Somaliland kama taifa huru, na inalitizama kama sehemu muhimu ya maeneo yake, na kuona kujihusisha moja kwa moja nao ni ukiukwaji wa uhuru na umoja wa nchi ya Somalia.