Rais wa Vikoba endelevu Tanzania Mohamed Basanga amewataka wanachama wote wa Vikoba Tanzania kuhakikisha wanavitumia Kujiletea Maendeleo ya Kiuchumi na Kukuza hali ya Kipato cha familia na Taifa kwa Ujumla.
rais Basanga amezungumza hayo jijini Dar es saaalm katika sherehe ya kufunga Mwaka 2025 na kuukaribisha mwaka 2026 iliyoandaliwa na taasisi ya Sevior Vikoba endelevu ambapo amesema mfumo na muundo wa vikoba kuna kila nyenzo inayomuezesha mwanachama kufanya shughuli za kuboresha maisha yake.
Naye Mwanzilishi wa Sevior Vikoba endelevu Tatu Pokela amesema mpango wa sasa ni kuviunganisha vikundi hivyo na mifuko rasmi ya uwekezaji yenye hisa kwa manufa ya wanachama.