
Akizungumza katika kikao cha dharura cha bunge, Rais wa Somalia Hassan Sheikh Mohamud amesema serikali yake haitokubali kamwe uamuzi wa Israel akiueleza kuwa unakiuka wazi mamlaka na mipaka ya Jamhuri ya Shirikisho la Somalia.
Amesema Somalia itatumia njia zote za kidiplomasia kulinda mamlaka yake, akitaja hatua ya Israel kuwa uchokozi unaotishia si tu Somalia bali pia uthabiti wa eneo zima.
Hatua ya Israel imezidisha wasiwasi kutokana na nafasi ya kimkakati ya Somaliland karibu na Lango la Bab al-Mandab ambalo ni muhimu kwa usafiri wa baharini linalounganisha Bahari ya Shamu na Ghuba ya Aden.