Vita vinavyoendelea kati ya Urusi na Ukraine vinaendelea kuathiri moja kwa moja nchi za Afrika, hususan katika upatikanaji wa bidhaa muhimu kama ngano na mafuta.

Mchambuzi wa siasa Abdulaziz Jaad, kutoka Uingereza, anasema mgogoro huo umevuruga minyororo ya ugavi duniani, kupandisha bei za bidhaa na kuongeza gharama za maisha barani Afrika.

Kwa upande wake, mchambuzi Ibrahim Rahbi anabainisha kuwa mataifa mengi ya Afrika ni wategemezi wakuu wa bidhaa zinazozalishwa na nchi hizo mbili, hivyo vita imeleta uhaba sokoni, kuongeza presha kwa uchumi na kuhatarisha usalama wa chakula.

Wataalamu wanashauri Afrika kuongeza uzalishaji wa ndani na kupunguza utegemezi ili kujenga uthabiti wa kiuchumi endapo mgogoro huo utaendelea

✍ Ibrahim Kilumbo
Mhariri | @claud_jm
#AzamTVUpdates

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *