OFISA Habari wa Klabu ya Young Africans, Ali Kamwe, amezua mjadala katika mitandao ya kijamii baada ya kuchapisha ujumbe unaogusia uwezekano wa kurejea mahusiano yake ya zamani.

Ujumbe huo wa Kamwe umekuja wakati kukiwa na taarifa za kurejeana kwa msanii wa muziki wa kizazi kipya, Rajab Abdul ‘Harmonize’ na mwigizaji Frida Kajala. SOMA: Kamwe: Tutachukua hatua kunyimwa goli jana

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Ali Kamwe aliandika,”Mtu yeyote niliyewahi kuwa naye katika mahusiano hapo awali na anahisi kunikumbuka, naomba anitafute tujadiliane kwa kina”alimalizia.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *