Nchini Ivory Coast, chama tawala chake rais Allasane Ouattara, RHDP kimepata ushindi kwenye uchaguzi wa wabunge uliofanyika mwishoni mwa wiki iliyopita.

Imechapishwa: Imehaririwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Ushindi huu, unatarajiwa kumpa nguvu rais Ouattara, kupitisha ajenda za serikali yake bungeni.

Matokeo hayo yamekiacha chama kikuu cha upinzani, kikiongozwa na Tidjane Thiam, na viti pungufu baada ya uchaguzi huo muhimu.

Katika uchaguzi huo, chama cha Ouattara kimepata ushindi wa viti 197 kati ya 255 vilivyokuwa vinawaniwa katika uchaguzi huo.

Rais wa Côte d'Ivoire
Rais wa Côte d’Ivoire via REUTERS – SIA KAMBOU

Chama upinzani cha PDCI, kimepata viti 32, kutoka viti 65 kama ilivyokuwa hapo awali, huku wabunge 23 wakichaguliwa kwa tiketi binafsi.

Tume ya uchaguzi imesema, asilimia 35.04 ya wapiga kura walijitokeza kwenye uchaguzi huo, ukilinganishwa na asilimia 37.8 ya wapiga kura waliojitokeza mwaka 2021.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *