#HABARI: Waombaji 14,433 wamechaguliwa kujiunga na mafunzo ya ufundistadi VETA kwa mwaka wa masomo 2026 kati ya 18,875 waliowasilisha maombi wakiwemo 134 ambao ni wahitimu wa elimu ya juu wenye Astashahada, Shahada, Shahada ya Uzamili pamoja na watu wenye ulemavu.

Akizungumza jijini Dodoma Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) CPA Antony Kasore amesema uchaguzi wa wanafunzi hao umezingatia uwezo wa vyuo vya VETA, fani walizoomba na Sera ya kutoa kipaumbele kwa wanawake pamoja na watu wenye mahitaji maalum ambao wamechaguliwa 145 kati ya 195 walioomba na mafunzo yao yatagharamiwa na Serikali.

Alisema kati ya waombaji hao,145 tayari wamechaguliwa kujiunga na vyuo 53 vya VETA na wengine 50 wanasubiri kupangiwa ikiwa waliojitokeza kuomba fani wana changamoto mbalimbali zikiwemo uoni hafifu, usikivu hafifu na ulemavu wa viongo ambapo wameonyesha uthubutu na Serikali imeamua kugharamia asilimia 100 ya masomo yao.

Powered by #MCHEZOSUPA

JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:

Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.

#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
#Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *