Nchini DRC, hali bado ni ya wasiwasi katika maeneo kadhaa karibu na mji wa Uvira, ambapo mapigano yanayoendelea kati ya jeshi la Kongo na waasi AFC/M23 wanaosaidiwa Rwanda, yamesababisha watu zaidi kukimbia makazi yao.

Imechapishwa: Imehaririwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Siku Jumatatu, milipuko ya mabomu na milio ya risasi ilisikika huko Uvira kufuatia mapigano katika maeneo ya Kigongo, Kabimba, Gomba na Katogo, takriban kilomita 8 kusini na kusini magharibi mwa Uvira. Stella, mkazi wa Uvira, ana wasiwasi.

“Mara tunasikia milio milimani upande wa Kalundu, mara mitaani … Hakuna kwa kukimbilia. Zikilia, kila mtu anajifungia nyumbani mwake. Na kuna wanaotembea huku milio ikisikika”

Vurugu za kiusalama zinaathiri pia hali ya kibinadamu kwa maelfu ya watu waliokimbia makazi yao katika eneo hilo. Nyenge Sango ni miongoni, anaelezea mazikitiko.

“Mimi niliamuwa kutoka Baraka hadi hapa Uvira na sasa tunalala kanisani. Watu wanahangaika, hakuna maji, watu wanatumia maji ya ziwa Tanganyika, wengine wanatumia maji ya nvuwa … Hii ni shida kabisa. Ikiwa kutakuwa na uwezekano kabisa, juhudi zifanyika huu mzozo umalizike”

Kelvin Bwija ni mwanaharakati wa asasi yakiraia iitwayo SOCICO mjini Uvira, anatoa onyo kwa pande hasimu :

“Hadi sasa mapambano bado yanaendelea. (M23) hawaheshimu mikataba yakutafuta amani mashariki mwa Congo. Tunaomba viongozi wajifunze mbinu fulanifulani za kulinda usalama wa raia”

Asasi za kiraia zinashuhudia pia uharibifu wa miundombinu kadhaa ya afya na elimu kufuatia mapigano hayo.

William Basimike, Bukavu, RFI Kiswahili 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *