Kufunguliwa tena kwa Jumba la Makumbusho Taifa la Libya baada ya kufungwa kwa miaka 14 kunatoa matumaini ya kurejea utulivu nchini humo na kujumuishwa utambulisho wa kitaifa.

Baada ya Makumbusho ya Taifa ya Libya kufungwa kwa muda wa miaka 14 kutokana na vita vya ndani, hatimaye jumba hilo la makumbusho limefunguliwa na kutoa fursa kwa wageni kuchunguza na kufahamu historia tajiri na changamani ya Libya.

Nchi hiyo ya tajiri kwa mafuta ya Mediterania imepambana kulinda turathi zake dhidi ya historia ya vita, machafuko na ukosefu wa amani miaka kadhaa, hata hivyo kufunguliwa tena kwa makumbuhso hayo makubwa huko Tripoli kunatoa mwanzo mpya na wa matumaini.

Kamal Yousef Mkurugenzi wa utawala wa Makumbusho ya Taifa ya Libya anasema:  Makumbusho hayo ni “ngome ya kitamaduni” inayohifadhi historia nyingi za Libya katika jengo moja.

Ameongeza kuwa: Wakati jengo hilo la makumbusho ya taifa lilipokuwa limefungwa na nchi ikiwa katika machafuko walichukua chukua tahadhari ili kulinda vitu na turathi za kale ambapo hakuna wizi uliojiri.

Jumba hilo la makumbusho lina sanamu nyingi za kihistoria za Kigiriki na Kirumi,  turathi nyingi za kale kutoka maeneo mbalimbali ya Libya n.k.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *