
Takwimu rasmi zinaonyesha ukuaji wa mauzo ya nje ya Iran kwa nchi za Afrika katika miezi minane iliyopita.
Mohammad Reza Safari, Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Afrika ya Shirika la Maendeleo ya Biashara la Iran, ametangaza kwamba kiasi cha biashara ya Iran na nchi za Afrika kimefikia dola milioni 849 katika miezi minane iliyopita, ambayo ni ongezeko la asilimia 77 ikilinganishwa na kipindi kama hicho mwaka jana (1404 Hijria Shamsia).
Safari ameongeza kuwa kiasi hiki cha mauzo ya nje ni sawa na jumla ya mauzo ya nje ya Iran barani Afrika mwaka jana. Kulingana na Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Afrika ya Shirika la Maendeleo ya Biashara la Iran, Kenya, Ghana, Afrika Kusini, Somalia na Tanzania zilikuwa sehemu muhimu zaidi za mauzo ya nje ya Iran.