#MICHEZO: Mbunge wa Jimbo la Mbulu Vijijini, Dr. Emmanuel Nuwas, amezindua rasmi mashindano ya Kombe la Waamuzi wa Mpira wa Miguu Tanzania (Referee Cup 2025). Uzinduzi huo umefanyika katika Uwanja wa Tanzanite Kwaraa, ambapo waamuzi kutoka mikoa mbalimbali nchini wamekusanyika kuchuana uwanjani.

Lengo kuu la mashindano haya ni kudumisha umoja na mshikamano miongoni mwa waamuzi wa Tanzania. Badala ya kusimamia sheria kama walivyozoeleka, safari hii waamuzi wenyewe wameingia dimbani kusakata kabumbu, jambo ambalo linajenga urafiki na ushirikiano nje ya majukumu yao ya kila siku ya kikazi.

Akizungumza wakati wa uzinduzi huo, Dr. Nuwas amewapongeza waamuzi hao kwa hatua hiyo ya kipekee. Alisisitiza kuwa waamuzi wana mchango mkubwa sana katika ukuaji wa soka la Tanzania, na kuwataka waendelee kuwa na weledi na mshikamano ili kuendeleza mchezo huo nchini.

Powered by #MCHEZOSUPA

JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:

Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.

#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *