Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Anamringi Macha ameuagiza uongozi wa Halmashauri Wilayani Busega kuchukua hatua madhubuti ikiwemo kuwatafutia eneo mbadala Wananchi wanaofanya shughuli zao za biashara katika Soko la Kisesa Kata ya Lamadi ili kuepusha madhara zaidi yanayoweza kusababishwa na mvua zinazoendelea kunyesha zizilizolelekea kufurika kwa mto Lamadi.

Ametoa maagizo hayo katika ziara yake Wilayani humo kukagua maeneo mbalimbali yaliyoathiriwa kutokana na kujaa kwa mto Lamadi kufuatia mvua zinazoendelea kunyesha katika maeneo mbalimbali Nchini.

Aidha Macha ameuagiza uongozi wa Halmashauri kusitisha shughuli za kibinadamu zinazofanyika ndani na pembezoni mwa Mto Lamadi pamoja na kufanyika kwa usafi haraka katika mto huo ili kuepusha hatari za magonjwa ya malipuko.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *