MKUU wa Wilaya ya Kahama, Frank Nkinda amesema ni muhimu madiwani wakafahamu masuala ya itifaki na utawala bora ili kuepuka migogoro ikiwemo kusimamia vyema maendeleo ya miradi inayokwenda kutekelezwa.

Nkinda amesema hayo alipokuwa akifungua semina elekezi ya siku tatu kwa madiwani wa Halmashauri ya Manispaa ya Kahama yaliyotolewa na Chuo cha Serikali za Mitaaa Hombolo kwa kusimamiwa na Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi).

Nkinda amesema mada ya itifaki na maadili ambayo watajifunza madiwani ni muhimu kwani walio wengi.

“Tumieni mioyo yenu na mikono yenu kutenda mema kwa wananchi waliowachagua. Wana changamoto nyingi muache alama ili kila mwananchi aweze kuwafurahia na itifaki lazima ifuatwe ili kuepusha migogoro,”amesema Nkinda.

Nkinda amesema madiwani waachane na siasa za chuki wapendane na wasiogope huku wakifanya kazi kwa maslahi ya wananchi waliowachagua.

Ofisa Tawala Msaidizi kutoka ofisi ya Waziri Mkuu Tamisemi, Mashaka Makika amesema mada za mafunzo yanayotolewa kwa madiwani walio wengi wapya ni sheria, majukumu na muundo wa serikali za mitaa, mipango na bajeti, usimamizi wa miradi na ardhi, haki na wajibu ikiwemo maadili kwa madiwani.

Mkurugenzi wa Manispaa ya Kahama, Masud Kabetu amesema madiwani hao mwezi Januari wanakwenda kwenye vikao hivyo wanatakiwa kujua utaratibu wa vikao, maadili ya viongozi, utawala bora na shughuli nzima za uendeshaji halmashauri.

Mstahiki Meya wa Manispaa ya Kahama, Mataruma Kaniki amesema matarajio ya semina hiyo madiwani kuzingatia usimamizi mzuri kwenye miradi iliyopo katika maeneo yao.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *