Uwepo wa changamoto ya ajira katika jamii umeleta ubunifu na kuibua vipaji kwa wahitimu wa elimu ya juu, ambapo wahitimu wamekuwa wakijiunga na elimu ya vyuo vya kati VETA ili kupata mafunzo na ujuzi wa kujiiingizia kipato.

Shalom Ibrahimu, muhitimu wa shahada ya masuala ya Uchumi na Fedha, alianza na biashara ndogo ndogo za kuuza juice na pili pili kabla ya kujiunga na elimu ya VETA kusomea Uzalishaji wa chakula (Food Production), hatua iliyomsaidia kuajiriwa katika hoteli kubwa hadi kufikia hatua ya kujiajiri.

Msikilize muhitimu huyu akisimulia namna masomo ya VETA yalivyomletea mafanikio.

✍ Halima Abdallah
Mhariri | @claud_jm
#azamtvupdates

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *