Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu – Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Prof. Riziki Shemdoe, amewaagiza Wakuu wa Mikoa, Makatibu Tawala wa Mikoa, Wakuu wa Wilaya pamoja na Wakurugenzi wa Halmashauri kuhakikisha hakuna mtoto anayezuiwa kuanza au kuendelea na masomo kwa sababu ya kukosa sare, wakati shule nchini zikitarajiwa kufunguliwa Januari 13, 2025.

Prof. Shemdoe amesema agizo hilo linapaswa kusimamiwa kikamilifu katika maeneo yote ya nchi ili kuhakikisha kila mtoto anapokelewa shuleni bila masharti yanayokiuka miongozo na sera za elimu.

Aidha, Prof. Shemdoe amekemea tabia ya baadhi ya shule za Serikali kuweka michango mingi kwa wazazi, ikiwemo kuwalazimisha kununua sare shuleni, akieleza kuwa hatua hiyo ni kinyume na taratibu na miongozo ya Serikali.

Shemdoe amewaelekeza walimu wakuu, walimu na viongozi wa shule kusoma, kuelewa na kuzingatia miongozo ya elimu iliyopo, pamoja na kutoa elimu sahihi kwa wazazi na walezi ili kuondoa sintofahamu zisizo za lazima kwakuwa lengo la Serikali ni kuona watoto wote wanakwenda shule.

#kilichoborakabisa

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *