Timu ya taifa ya Senegal imefanikiwa kufuzu hatua ya 16 bora ya michuano ya AFCON inayoendelea nchini Morocco na kumaliza wa kwanza kwenye Kundi lake, ushindi huo sasa ukifanya DRC kucheza hatua inayofuata na miamba Algeria, huku Tanzania kwa mara ya kwanza kwa zaidi ya miaka 45 ikifuzu hatua ya 16 bora kufuatia sare ya bao 1-1 na Tunisia.

Imechapishwa: Imehaririwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Senegal wamefuzu hatua hiyo baada ya kupata ushindi mnono wa mabao 3-0 dhidi ya Benini katika mchezo wa Kundi D, huku DRC wao pia wakichomoza na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Botswana, Leopard ikimaliza ya pili kwa alama 7 sawa na Senegal lakini zikitofautiana kwa mabao ya kufunga na kufungwa na vinara wa Kundi Senegal.

Wachezaji wa Leopard wakati wa mechi yao dhidi ya Botswana.
Wachezaji wa Leopard wakati wa mechi yao dhidi ya Botswana. AP – Mosa’ab Elshamy

Katika mechi za Kundi C, Tanzania wameandika historia baada ya kufuzua hatua hiyo kama best looer kwenye Kundi lake, kufuatia sare ya bao 1-1 na Tunisia, sare hiyo ikiwatupa nje ndugu zao Uganda ambao walikubali kipigo cha mabao 3 – 1 toka kwa Nigeria iliyomaliza kinara wa Kundi kwa alama 9 ikifuatiwa na Tunisia yenye alama 4 na Tanzania alama 2.

Mashabiki wa Taifa Stars wakati wakifuatilia mechi yao dhidi ya Tunisia jijini Rabat nchini Morocco.
Mashabiki wa Taifa Stars wakati wakifuatilia mechi yao dhidi ya Tunisia jijini Rabat nchini Morocco. REUTERS – Stringer

Kwa matokeo haya, Mali sasa watacheza na Tunisia siku ya Jumamosi, huku Tanzania wakikabiliwa na kibarua kigumu dhidi ya wenyeji Morocco siku ya Jumapili. Aidha Jumatatu Misri watacheza na Benin, huku Jumanne DRC watakuwa na kibarua dhidi ya Algeria.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *