Chanzo cha picha, Sky Sport
Muda wa kusoma: Dakika 4
Ilionekana kama Arsenal wameanza kuyumba. Baada ya kuanza mwezi Desemba kwa kushindwa na Aston Villa, na waliwashinda Wolves, Everton na Brighton kwa tofauti ndogo ya magoli.
Lakini Gunners walipata matokeo mazuri na wakaondoa mashaka yote yaliyokuwepo kwa ushindi mzito wa nyumbani dhidi ya Villa 4-1 siku ya Jumanne.
Arsenal inaelekea mwaka 2026, na kipindi cha pili cha msimu, wakiwa kileleni mwa ligi kuu England – wakiwa mbele kwa pointi tano dhidi ya Manchester City walio katika nafasi ya pili, huku Villa wakiwa nyuma zaidi.
“Arsenal kufanya walichofanya kwa Villa maana yake ni kuwa kila kitu kinakwenda sawa kwa sababu kila mtu anachangia – meneja, wachezaji na wafanyakazi,” anasema mshambuliaji wa zamani wa Aston Villa, Dion Dublin.
Akizungumza kwenye kipindi cha Match of the Day cha BBC, kiungo wa zamani wa Uingereza, Danny Murphy aliongeza: “kiwango cha Arsenal kinatoa kauli kubwa juu ya nguvu, ubora na uimara wao.”
Lakini wana historia ya kukosa taji kwa kumaliza katika nafasi ya pili mara tatu mfululizo. Je, Arsenal itaweza kuwa mabingwa msimu huu kwa mara ya kwanza tangu 2004?
‘Ni wakati wa wasiwasi?’
Arsenal wamewahi kufika hapa walipo leo. Mwaka 2023 walikuwa nafasi ya juu, pointi tano juu ya Manchester City.
Lakini meza ilipinduliwa na kikosi cha Pep Guardiola ndicho kilichokuwa kinashikilia kombe mwishoni mwa msimu baada ya kumaliza pointi tano mbele ya Gunners.
Ilikuwa hadithi kama hiyo katika msimu wa 2002-03, walipomaliza pointi tano nyuma ya Manchester United baada ya kuwa kileleni mwishoni mwa Desemba.
Katika mara zote sita ambapo Arsenal walimaliza mwaka wakiwa katika nafasi ya kwanza, wameshinda Ligi Kuu mara moja tu – mwaka 2001-02.
Hiyo ni sababu ya msingi kwa nini mashabiki wao wana tahadhari kuhusu kusherehekea mapema.
“Inaeleweka sababu – ni karibu miaka 22 bila taji la ligi,” mlinzi wa zamani wa Liverpool Jamie Carragher alisema kwenye Sky Sports.
“Lakini wakati wa kuwa na wasiwasi ni Aprili na Mei, si sasa. Kuna safari ndefu bado.”
Historia inaonyesha, timu ambayo iko juu ya jedwali mwishoni mwa mwaka na kushinda Ligi Kuu msimu huo, imetokea mara 17 kati ya 33 (52%).
‘Tunajua tunachotaka’

Bosi wa Arsenal, Mikel Arteta aliambia BBC Sport: “Tunajua tunachotaka kuanzia 2026, tutalazimika kukipata na bado tuna safari ndefu mbeleni.”
Mafanikio dhidi ya Villa yalikuwa mara ya kwanza tangu Desemba 8 ambapo Gabriel na William Saliba walianza mchezo wakiwa mabeki wa kati pamoja.
Hata wawili hao wakiwa nje ya uwanja, Arsenal wana safu nzuri ya ulinzi katika ligi, wakiruhusu mabao 12 pekee katika michezo 19 – idadi ndogo zaidi kuliko timu yoyote.
Dhidi ya Villa, wawili hao walionyesha mchezo mzuri, ingawa bila bao katika kipindi cha kwanza kabla ya Gabriel, Mbrazili kuanza kufunga bao la kushtukiza dakika tatu baada ya kuanza tena kwa mchezo.
“Arsenal hawaogopi – wanawaamini mabeki wao,” anasema kiungo wa zamani wa Liverpool, Danny Murphy kuiambia BBC Sport.
“Ushirikiano wa Saliba na Gabriel, uliwapa nafasi ya kuoyesha kuwa haogopi. Hilo ndilo unalolipata kutoka kwa hao wawili, mchezo mzuri na utulivu.”
Wapinzani wa Arsenal
Kama Arteta alivyosema, kuna “safari ndefu” – na City na Villa zote mbili ziko za moto karibu na Arsenal.
Timu ya Guardiola, ambayo imeipiku Gunners na kushinda kombe la Ligi Kuu mara mbili tangu Arteta alipochukua nafasi hiyo mwaka 2019, itakuwa nyuma kwa pointi mbili ikiwa itashinda dhidi ya Sunderland siku ya Alhamisi.
Villa, ambao walishinda mechi 11 mfululizo kabla ya safari yao kwenda Emirates na kufungwa. Bosi wao Emery atataka kuendelea kushinda.
“Ni mara ya kwanza Arsenal kuwashinda wapinzani wao wa kweli msimu huu, jinsi walivyoshinda na kiwango chao katika kipindi cha pili. Waliiangamiza kabisa Aston Villa.”