
Taarifa ya WHO Kanda ya Ulaya iliyochapishwa kwenye wavuti wake inasema kauli hiyo inafuatia utafiti uliofanywa na shirika hilo na wadau katika nchi 7 za Ulaya ukionesha kuwa virusi SARS-CoV-2, vinavyosababisha coronavirus“>COVID-19 vimeendelea kuwa ‘mwiba’ kwa watu kulazwa hospitalini na hata kufa.
Ingawa hivyo utafiti huo umethibitisha kuwa kupata chanjo ya COVID-19 kumesalia kuwa jawabu fanisi la kuepusha ugonjwa huo.
Miaka 6 iliyopita, tarehe 31 mwezi Desemba mwaka 2019, wagonjwa wa kwanza kuripotiwa kuugua vichomi au numonia huko waliripotiwa kwenye wavuti ya Kamisheni ya Afya ya Manispaa ya Wuhan nchini China na wagonjwa hao ndio ulikuwa mwanzo wa ripoti za janga la COVID-19.
“Takribani miaka 3 na nusu baadaye, yaani mwezi Mei mwaka 2023, baada ya takribani vifo vya zaidi ya watu milioni 6.9 duniani kote kutokana na COVID-19, WHO ilitangaza kuwa ugonjwa huo si tishio tena la afya ya umma, ingawa sasa inaonekana unaendelea kuua watu,” imesema WHO, kwenye taarifa yake.
Ni kwa mantiki hiyo WHO kanda ya Ulaya inaendelea kushirikiana na nchi wanachama na wadau wa ukanda wa Mashariki kuimarisha ufuatiliaji wa maambukizi ya njia ya hewa kupitia mtandao wa hospitali za kikanda uitwao EuroSAVE, ulioanzishwa mwaka 2021.
Nchi husika ziko maeneo ya Balkani, Asia ya Kati na Ukanda wa Kusini.
Matokeo ya utafiti
Mtandao wa EuroSAVE ulihusisha nchi 6 na kubaini kuwa kati ya wagonjwa 4000 waliolazwa kwa maambukizi makali ya njia ya hewa kati ya Mei 2023 na Aprili 2024 baada ya janga kutangazwa kuwa limemalizika, asilimia 10 walikuwa wanaugua COVID-19.
Utafiti huo ulibaini kuwa zaidi ya theluthi mbili ya wagonjwa waliolazwa walikuwa na umri wa zaidi ya miaka 60 na theluthi moja walikuwa na magonjwa sugu, na ndipo sasa “WHO inapendekeza wawe wanapatiwa chanjo ya COVID-19 kila mwaka.”
Hata hivyo asilimia 3 ya wagonjwa waliolazwa walikuwa wamepatiwa chanjo ya COVID-19 katika kipindi cha miezi 12 iliyotangulia.
“Tafiti zetu zikitumia takwimu kutoka mtandao wa EuroSAVE zinadokeza kwamba, ilhali COVID-19 haiongozi katika kusambaa kwa ugonjwa kama ilivyokuwa wakati wa janga, bado imekuwa ikiwa sababu kubwa ya watu wengi kulazwa hospitali na kufa. Zaidi yah apo, madhara ya virusi yanaendelea kuonekana kuwa makali n ahata kuliko homa ya mafua,” amesema Dkt. Mark Kats, mtaalamu wa magonjwa ya kuambukiza na usugu wa viuavijisumu huko WHO Kanda ya Ulaya.
Kupatiwa chanjo
Wakati huu COVID-19 ikiendelea kusababisha vifo, WHO inaendelea kusisitiza umuhimu wa kuwapatia upya chanjo watu walio kwenye makundi hatarishi kama vile wazee, wajawazito na wahudumu wa afya.
Soma taarifa nzima hapa.