
Mapigano mapya yamezuka kati ya waasi wa AFC/M23 na wapiganaji wa Wazalendo, wanaoungwa mkono na jeshi la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, katika wilaya za Masisi na Walikale.
Imechapishwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Kuanzia siku ya Jumanne, mapigano makali yameshuhudiwa katika eneo la Nzanganano, karibu na Minjenje, kwa mujibu wa rpoti za mashirika ya kiraia na wakaazi wa maeneo hayo.
Ripoti zaidi zinasema, wapiganaji wa Wazalendo, ndio walionekana katika eneo hilo kuanzia majira ya asubuhi na kusababisha mapigano hayo ambayo yamewaacha wakaazi wa kijiji cha Nzanganano, wakiishi kwa hofu.
Siku ya Jumatano, hali imeripotiwa kuwa tulivu lakini kuna wasiwasi katika kijiji hicho ambacho kinadhibitiwa na waasi wa AFC/M23, baada ya wapiganaji Wazalendo kujiondoa.
Katika hatua nyingine, hali ya wasiwasi imeendelea kushuhudiwa mjini Uvira, huko Kivu Kusini, licha ya waasi wa M23/AFC kuondoka Desemba tarehe 16.
Uchumi wa mji huo umeyumba, kufuatia kufungwa kwa mpaka wa nchi jirani ya Burundi, na kuwafanya wakaazi kushindwa kuendelea na shughuli zao za kawaida.