Vipindi vya ukame na mvua kubwa vimesababisha uharibifu wa mashamba na mafuriko. Lakini kupitia mradi huu wa BRiMS, mifereji 126 yenye urefu wa km 240 imejengwa na imenufaisha zaidi ya ekari 22,000 katika maeneo ya Beledweyne na Jowhar, ikilinda jamii na kusaidia wakulima kama Amina Ibrahim Moalim kulima tena na kustahimili mabadiliko ya tabianchi.

Mafuriko yaliharibu mashamba yetu ya mahindi, maharagwe na mboga. Kwa msaada wa FAO, sasa tunaweza kulima tena na kuhimili athari za mabadiliko ya tabianchi.

Ili kuhakikisha usimamizi bora wa maji na kupunguza hatari za mafuriko, FAO  imeandaa na kutoa mafunzo kwa kamati 9 za watumiaji wa maji, zikisaidia jamii kusimamia upatikanaji wa maji, matengenezo ya mifereji, na kutatua migogoro kwa ufanisi. Ahmed Nur Hassan ambayeanahusika na ugawaji wa maji anasema

Nimehudumia jamii yangu tangu mwaka 1992. Shukrani kwa mafunzo na miundombinu ya FAO, sasa tunapata maji hata wakati wa ukame.”

Ili kuimarisha kilimo, vyama 7 vya wakulima vimeanzishwa na kupewa mafunzo na vifaa. Shirikisho la Al-Cadaala lenye wanachama 750 linaongoza kusimamia uzalishaji, maji na masoko. Hodan Ahmed Hassan, ni Mwenyekiti wa Shirikisho la Al-Cadaala anasema

Kawaida tulipigana kwa ajili ya maji. Sasa tuna miundo, mafunzo, na amani. Shirikisho letu ni hadithi ya mafanikio.”

Kwa mujibu wa FAO, Mradi wa BRiMS umewezesha wakulima 7,000 kulinda mazao na kujenga maisha bora, lakini msaada endelevu ukihitajika ili kupanua zaidi umwagiliaji, mafunzo, na masoko kwa maelfu zaidi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *