
Kufuatia ziara ya Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu huko Washington, Rais wa Marekani Donald Trump aliongeza shinikizo kwa Hamas. Aliahidi kwamba kundi hilo lenye silaha lingelipa “gharama kubwa ikiwa halitasalimisha silaha zao” kama sehemu ya awamu ya pili ya makubaliano ambayo Washington ilisaidia kuratibu mwaka huu. Kuhusu miradi ya ujenzi upya wa Gaza, ambayo pia imepangwa katika awamu hii ya pili, raia wa eneo hilo hawakushirikishwa kwa njia yoyote.
Imechapishwa:
Dakika 2 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Na mwandishi wetu huko Gaza, Rami El Meghari, akishirikiana na mwandishi wetu wa kitengo cha kimataifa, Aabla Jounaidi
Maisha ya kila siku ya Wapalestina huko Gaza ni yanazidi kuwa mabaya. Katika kambi ya muda kando ya bahari, Umm Ahed, mwenye umri wa miaka hamsini, anatoka kaskazini na anasubiri jambo moja tu: misafara. “Mahema haya madogo wanayotupa yalipeperushwa na upepo ambao tumeshuhudia siku chache zilizopita,” anasema. “Usiku, watu hupiga kelele kwa sababu maji hupanda juu na kusomba kila kitu, ikiwa ni pamoja na mahema na samani. Tunataka makazi imara zaidi, kwa sababu tutakuwa hapa kwa miaka ijayo—miwili, mitano, au labda kumi!”
Hamdi Ali, kwa upande wake, hatarajii chochote kutoka kwa mazungumzo yanayoendelea. Wasiwasi wake pekee ni kutoa mahitaji kwa familia yake ya watu wanane. “Hatujui kinachotusubiri. Tuna hofu iya hali kuwa mbaya zaidi. Tunamtumaini Mungu tu sasa. Nchi za kigeni zinatudhihaki,” Mpalestina huyu amesema .
Changamoto za kiufundi, vifaa, na kiuchumi
Hata baada ya ziara ya Waziri Mkuu wa Israel katika Ikulu ya White House siku ya Jumatatu, Desemba 29, mustakabali wa Gaza bado haujajulikana. “Bado kuna nia hii kwa upande wa Marekani ya kuendeleza miradi yake ya kimkakati na kiuchumi katika eneo hilo.” Hili ndilo linalopaswa kuwezesha kudumisha usitishaji mapigano na kisha ujenzi upya huko Gaza. Lakini yote haya yanahatarishwa na changamoto za kiufundi na vifaa; masuala ya kifedha bado hayajatatuliwa, bila kusahau hitaji la kuwajali watu wote hapa,” anaelezea profesa na mtaalamu wa masuala ya siasa na uchumi Mohamed Abou Jiab.
Mamlaka ya Israel imeamua kwamba hii haitakuwa hivyo. Mashirika 37 yasiyo ya kiserikali ya kimataifa yamepigwa marufuku kufanya kazi Gaza kufikia Januari 1, 2026. Makubaliano dhaifu ya kusitisha mapigano yamekuwa yakiendelea Gaza tangu mwezi Oktoba, kufuatia vita vikali kati ya jeshi la Israel na Hamas. Lakini mgogoro wa kibinadamu unatishia wakazi wake milioni 2.2.