#HABARI: Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, limetoa tahadhari kali kwa wananchi dhidi ya vitendo vya kuchoma matairi barabarani pamoja na kupiga baruti au fataki katika maeneo yasiyoidhinishwa, likisisitiza kuwa watakaobainika kufanya vitendo hivyo katika kipindi cha sherehe za Mwaka Mpya watachukuliwa hatua za kisheria mara moja.
Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, SACP Jumanne Muliro, amesema Jeshi la Polisi lina jukumu la kuzuia na kudhibiti vitendo vya kihalifu katika maeneo mbalimbali ya Jiji la Dar es Salaam kuelekea maadhimisho ya Mwaka Mpya, kwa kushirikiana na vyombo vingine vya ulinzi na usalama.
Amesisitiza kuwa hatua zitachukuliwa kwa haraka kwa mtu au kikundi chochote kitakachobainika kukiuka marufuku hiyo, huku Jeshi la Polisi likizingatia misingi na taratibu zote za kisheria katika utekelezaji wa majukumu yake.
Aidha, amesema Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam linaendelea kushirikiana kwa karibu na wananchi pamoja na viongozi wa nyumba za ibada ili kuhakikisha shughuli zote za ibada zinafanyika katika mazingira salama kipindi cha sikukuu. Kamanda Muliro pia amewakumbusha wananchi kuhakikisha makazi yao, ofisi na maeneo ya biashara hayabaki wazi bila uangalizi, hasa katika kipindi hiki cha sikukuu na nyakati nyingine za shughuli za kijamii na kiuchumi.
Powered by #MCHEZOSUPA
JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:
-
Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.
#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania.