‎#HABARI: Mali na Burkina Faso zimesema zinaweka marufuku ya kusafiri kwa raia wa Marekani, kama jibu la hatua sawia iliyotangazwa na utawala wa Trump mapema mwezi huu.

Katika taarifa tofauti zilizotolewa na wizara zao za mambo ya nje mwishoni mwa Jumanne, nchi hizo mbili za Afrika Magharibi zilisema zinachukua hatua hiyo kwa misingi ya kulipizana, baada ya Ikulu ya White House kutangaza Disemba 16 kwamba Rais wa Marekani Donald Trump alikuwa anaongeza nchi hizo pamoja na nyingine tano kwenye orodha ya nchi zitakazokumbwa na marufuku kamili ya kusafiri.

Ikulu ya White House ilisema kuwa marufuku hiyo iliyopanuliwa, inayotarajiwa kuanza kutekelezwa Januari 01, inahusu nchi zilizoonyesha mapungufu makubwa, ya kudumu na makali katika uchunguzi, uhakiki, na ushirikiano wa taarifa ili kulinda taifa dhidi ya vitisho vya usalama wa taifa na usalama wa umma.

Mali ilisema Jumanne kwamba uamuzi wa Washington wa kuiingiza kwenye orodha ya marufuku ya kusafiri ulifanywa bila mashauriano ya awali, na kwamba sababu iliyotolewa haikuthibitishwa na hali halisi ilivyo ardhini.

Mali na Burkina Faso si nchi za kwanza kuchukua hatua kama hizi zinazowaathiri raia wa Marekani baada ya kulengwa na vikwazo vya kusafiri vya Trump.

Desemba 25, jirani yao Niger ilitangaza kuwa ingeacha kutoa visa kwa raia wa Marekani, shirika la habari la Serikali ya nchi hiyo liliripoti, likinukuu chanzo cha kidiplomasia cha Niger.

Mwezi Juni, Chad ilitangaza kusitisha utoaji wa visa kwa raia wa Marekani baada ya kujumuishwa kwenye orodha ya awali ya nchi 12 zilizoathiriwa na marufuku ya kusafiri.

‎Powered by #MCHEZOSUPA


‎JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:
‎-
‎Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.

‎#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
‎Follow @itvtz @radioonetanzania
‎@capitaldigitaltanzania.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *