#HABARI: Waziri Mkuu wa zamani wa Bangladesh Khaleda Zia, ambaye wengi walidhani kuwa angeshinda katika Uchaguzi wa mwaka ujao kuongoza nchi yake kwa mara nyingine tena, amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 80.
Khaleda alikuwa na ugonjwa wa cirrhosis ya ini, kisukari, kifua na matatizo ya moyo, Madaktari wake walisema.
Licha ya miaka mingi ya afya mbaya na kifungo, Zia aliapa mwezi Novemba kufanya kampeni katika uchaguzi uliopangwa kufanyika Februari 2026, kura ya kwanza tangu vuguvugu la lililompindua mpinzani wake mkuu Sheikh Hasina mwaka jana.
Mwishoni mwa Novemba, alikimbizwa hospitalini, ambapo, licha ya juhudi kubwa za madaktari, hali yake ilizidi kuwa mbaya kutokana na msururu wa masuala ya kiafya.
Zia, alikuwa Waziri Mkuu wa Bangladesh kutoka mwaka 1991 hadi 1996, na tena kutoka 2001 hadi 2006. Alikuwa mwanamke wa kwanza kuhudumu kama Waziri Mkuu wa nchi hiyo.
Powered by #MCHEZOSUPA
JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:
–
Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.
#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
#Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania.