#HABARI: Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – Mipango na Uwekezaji, Profesa Kitila Mkumbo, ameutaja Mkoa wa Pwani kuwa kinara wa uzalishaji wa ajira Nchini kwa mwaka 2025, baada ya kuzalisha ajira 86,621, hatua inayodhihirisha utekelezaji mzuri wa vipaumbele vya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, hususan katika eneo la ajira.
Waziri Prof. Mkumbo amebainisha hayo wakati wa hafla ya makabidhiano ya hati za mikataba ya uwekezaji kwa wawekezaji waliopatiwa maeneo katika Eneo Maalum la Uchumi la Bagamoyo Eco Maritime City (BEMC SEZ), pamoja na utoaji wa Taarifa ya Hali ya Uwekezaji Nchini kwa mwaka 2025.
Powered by #MCHEZOSUPA
JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:
–
Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.
#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
#Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania.