Israel imetangaza kuwa inapiga marufuku mashirika 37 yakiwemo ya Kimataifa, yanayojihusisha  na kutoa misaada ya kibanadamu kwenye ukanda wa Gaza, kuanzia siku ya Alhamisi.

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Hatua hii imechukuliwa na Israel, ambayo inasema, mashirika hayo yameshindwa kuzingatia utaratibu mpya wa kutoa taarifa kuhusu wafanyazi wake, ambao ni Wapalestina.

Msemaji wa Wizara ya masuala ya diáspora iliyohusika pia kupambana na kupambana na kauli za chuki, Gilad Zwick amesema mashirika hayo licha ya kutakiwa kufuata utaratibu huo, yameshindwa na hivyo kufungiwa.

Aidha, Israeli inawashtumu baadhi ya wafanyakazi wa mashirika hao, kuhusika na matukio ya kigaidi, huku wengine wakishirikiana kwa karibu na kundi la Hamas.

Miongoni mwa mashirika hayo ni pamoja na lile la Madaktari wasiokuwa na mipaka, MSF ambalo limedaiwa kuwa na wafanyakazi wazwili ambao ni wanachama wa kundi la Kijihadi la Kiislamu na Hamas.

Mashirika mengine yaliyo kwenye orodha hiyo ni pamoja na Baraza la wakimbizi la Norway, World Vision International, CARE na Oxfam.

Uamuzi huu wa Israeli, umelaaniwa na Ofisi ya Haki za Binadamu ya Umoja wa Mataifa, inayosema, haikubaliki.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *