SIMBA kuna kazi moja inamaliziwa na wakati wowote kuanzia jana mpaka muda huu unaposoma gazeti hili itakuwa imemalizika kwenye kuunda benchi jipya la ufundi la kocha mpya wa wekundu hao Steve Barker.

Barker tayari yupo nchini akitua na watu wawili wa kazi ambapo sura ya benchi lake imeanza kutoa picha kwamba jamaa amekuja kupigania heshima ya Simba na yake binafsi

SIM 01

WASAIDIZI WAWILI

Barker atakuwa na makocha wawili wasaidizi ambapo wa kwanza atakuwa Maahier Fadlu ambaye ni mdogo wake aliyekuwa kocha wa timu hiyo Fadlu Davids.

Nyuma ya Maahier ambaye amewahi kufanya kazi Uarabuni na Afrika Kusini akiwa bado hajawasili nchini, kutakuwa na kocha mzawa Seleman Matola.

Matola ameshakutana na Barker kisha kupeana mrejesho wa awali kuhusu kikosi hicho, kwenye kikao kilichofanyika hoteli moja jijini Dar es Salaam.

SIM 02

MZAMBIA WA MAKIPA

Barker pia ametua na kocha Davies Phiri, raia wa Zambia, ambaye ndiye atakuwa kocha wa makipa wa wekundu hao, akiwa amewahi kuzitumikia klabu za Amazulu FC,Golden Arrows za Afrika Kusini na Kabwe Warriors ya kwao Zambia.

Phiri alikuwa sehemu ya wachezaji kwenye kikosi cha Zambia, kilichopoteza Nusu Fainali ya Mataifa Afrika (AFCON 1996) dhidi ya Tunisia kwa mabao 4-2.

SIM 03

MCHAMBUZI WA VIDEO

Kocha Barker ambaye anatua Simba akitokea Stellenbosch ya Afrika Kusini, pia ametua na mchambuzi wa video Prinil Deen ambaye amewahi kuzitumikia Mamelodi Sundowns na Chippa United zote za Afrika Kusini.

SIM 04

MAKOCHA WA VIUNGO WAWILI

Barker atakuwa na makocha wawili wa mazoezi ya viungo lakini kwasasa bado inaonyesha wapo watatu, yakisubiriwa maamuzi ya mabosi wa Simba kumaliza utata eneo hilo kwenye kikao cha kocha huyo na vigogo wa klabu hiyo.

Barker amemleta kocha mwingine wa mazoezi ya viungo Sibusiso Makhula kutoka Upington ya Afrika Kusini ambaye tayari ameshatua nchini,akiungana na Riedoh Berdien ambaye alikuwa hapo tangu enzi za utawala wa Fadlu, akigoma kuondoka kuachana na wekundu hao.

Hata hivyo Simba ilimuongeza kocha wa mazoezi Mohammed Mrishona ‘Xavi’ kwenye benchi hilo ambapo kwa sasa unasubiriwa uamuzi wa mabosi wa Simba na Barker kuamua hatma ya mtaalamu huyo kusalia au kurejea kwenye kikosi cha vijana ambako alikuwa kabla.

Xavi kwa sasa yupo nchini Morocco akiwa sehemu ya benchi la ufundi la kocha wa muda wa Taifa Stars, Miguel Gamondi.

Simba itaendelea na meneja Patrick Rweyemamu ambaye sasa atakuwa na majukumu yake kamili kufuatia cheo hicho kugawanywa kwenye makundi mawili, wakati wa kocha Dimitar Pantev aliyekuwa akitambuliwa kama meneja wa Wekundu hao lakini kitengo cha matibabu pia kitaendelea kuwa chini ya Dk Edwin Kagabo aliyefunga ndoa wikiendi iliyopita.

SIM 05

WASEPA ZAO MAPINDUZI

Simba itaondoka leo kwenda Zanzibar kushiriki wa michuano ya Kombe la Mapinduzi 2026 inayoendelea visiwani humo, Barker anataka maandalizi yawe huko kabla ya kurudi katika mechi za michuano ya Ligi Kuu Bara na Ligi ya Mabingwa Afrika ikiwa Kundi D pamoja na timu za Esperance ya Tunisia, Stade Malien ya Mali na Petro Atletico ya Angola.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *