Madereva wanaotumia barabara ya Mandela jijini Dar es Salaam wameendelea kulalamikia foleni kubwa inayosababishwa na utaratibu usio rafiki wa maegesho ya magari ya mizigo yanayoingia na kutoka katika bandari kavu iliyopo eneo la Relini.
Mapema leo adhuhuri, Adhuhuri Live imeshuhudia hali hiyo ambapo baadhi ya watumiaji wa barabara hiyo, hususan wanaosafiri kutoka maeneo ya Buguruni kuelekea Ubungo, wamelazimika kusimama kwenye foleni kwa zaidi ya nusu saa.
âJoseph Mpangala
Mhariri | @claud_jm
#AzamTVUpdates