Mamlaka ya Udhibiti wa Mbegu Bora nchini, TOSCI, imeanza zoezi la ukaguzi wa mawakala wa pembejeo za kilimo mkoani Rukwa, ambapo imechukua hatua ya kumfungia mmoja wa mawakala hao baada ya kubainika kujihusisha na vitendo vya udanganyifu.

Kwa mujibu wa mamlaka hiyo, wakala huyo alibainika kumsajili mkulima hewa aliyedaiwa kupokea mbegu za ruzuku ya Serikali zaidi ya tani 330, hatua iliyofanyika kinyume cha sheria na taratibu za usambazaji wa pembejeo za kilimo.

TOSCI imesema ukaguzi huo unalenga kuhakikisha mbegu bora zinazotolewa kwa wakulima zinawafikia walengwa halisi, kudhibiti mianya ya ubadhirifu, pamoja na kulindaslahi ya wakulima na Serikali.

✍Sammy Kisika
Mhariri | @claud_jm

#AzamTVUpdates

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *