Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Russia, Maria Zakharova amejibu vitisho vya hivi karibuni vilivyotolewa na Rais wa Marekani na Waziri Mkuu wa utawala wa Kizayuni wa Israel dhidi ya Iran.

“Russia inatoa wito kwa wachochei kuachana na hatua za kushadidisha mvutano mkabala wa Iran,” amesema Msemaji wa Wizara ya Mambo ya nje ya Russia, Maria Zakharova.

Shirika la habari la Izvestia lilimemnukuu Zakharova akisema kwamba, matamshi ya Israel kuhusu uwezekano wa mashambulizi ya kijeshi dhidi ya Iran ni yanaibua wasiwasi mkubwa.

Katika mkutano na waandishi wa habari pamoja na Waziri Mkuu wa utawala wa Israel, Benjamin Netanyahu tarehe 29 Disemba, Rais Donald Trump wa Marekani alidai kuwa Washington iko tayari kufanya mazungumzo na Tehran lakini chaguo la kutumia nguvu za kijeshi bado liko mezani.

“Natumai hawatajaribu kujijenga tena, kwa sababu kama watafanya hivyo, hatutakuwa na chaguo ila kumaliza haraka urutubishaji huo,” alisema Trump.

Wakati huo huo, Marais wa Iran na Russia wamefanya mazungumzo ya simu na kuchunguza hali ya sasa ya uhusiano wa pande mbili, sambamba na kujadili njia za kupanua zaidi ushirikiano kati ya Tehran na Moscow. 

Rais wa Iran, Masoud Pezeshkian aliutaja uhusiano wa Iran na Russia kuwa wa kimkakati na kusisitiza umuhimu wa kuendeleza makubaliano yaliyopo ili kupanua zaidi ushirikiano wa pande mbili.

Dakta Pezeshkian na Rais Vladimir Putin wa Russia wamesitiza haja ya kuendelea kwa mashauriano na uratibu thabiti ili kupanua uhusiano wa pande zote, wakionyesha nia yao ya pamoja katika kuinua ushirikiano hadi ngazi za juu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *