Mataifa ya Mali na Burkina Faso yamesema yatawazuia raia wa Marekani kuzuru mataifa hayo, ikiwa ni hatua ya kujibu Marekani baada ya kuorodhesha raia wa mataifa hayo mawili kama wale wasiostahili kuzuru Marekani.
Imechapishwa: Imehaririwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Hatua ya Mali na Burkina Faso inatokana na utawala wa Rais Donald Trump, kuorodhesha mataifa hayo miongoni mwa nchi ambazo raia wake wanazuiliwa kuzuru Marekani kutokana na changamoto za kiusalama.
Burkina Faso, kupitia Waziri wa Mambo ya Nje, Karamoko Jean-Marie, imesema inajibu hatua ya Marekani huku Mali ikisema kuna haja ya usawa na heshima kutumika katika kila hatua inayochukuliwa.

Aidha, mataifa hayo mawili yameeleza kusikitishwa kwake kutokana na kile yamesema Marekani ilichukua hatua hiyo bila mashauriano.
Hatua ya Mali na Burkina Faso inajiri baada ya nchi jirani ya Niger pia kuchukua hatua kama hiyo dhidi ya raia wa Marekani, mataifa hayo matatu yapo chini ya utawala wa kijeshi.
Aidha, Marekani ilitangaza vikwazo vya muda kwa raia kutoka Tanzania, Burundi, Nigeria, na Zimbabwe dhidi ya kuzuru Marekani.