
Rais wa Somalia kwa mara nyingine amelaani uchokozi wa utawala wa Kizayuni wa kutambua ramsi kujitenga Somaliland na maeneo mengine ya Somalia nakusisitiza kuwa, lengo la Israel ni kudhibiti njia muhimu na za kiistratijia za baharini kwenye eneo la Pembe ya Afrika.
Kwa mujibu wa shirika la habari la Tasnim, Rais Hassan Sheikh Mahmoud wa Somalia, ambaye ametembelea Uturuki baada ya kukutana na Rais Recep Tayyip Erdogan, alisema kuhusu hatua ya utawala wa Kizayuni kutambua kujitenga eneo la Somalia la Somaliland amesema: Utawala wa Israel unataka kuudhibiti njia za kimkakati za baharini za Pembe ya Afrika na kuwahamisha Wapalestina kutoka Ghaza na kuwapeleka Somaliland.
Amesema kwamba, Somaliland imekubali kuwapokea Wapalestina, kujiunga na Makubaliano ya Abraham na kuanzisha kambi ya kijeshi katika eneo hilo.
Ameongeza kwamba, njama hiyo ya utawala wa Kizayuni dhidi ya Somalia kupitia eneo la Somaliland si ya amani hata kidogo. Vilevile amefichua kwamba, utawala wa Kizayuni umekuwepo Somaliland tangu zamani na hatua za awali za kuitambua rasmi zilishachukuliwa zamani kwa siri, hivi sasa wametangaza hadharani tu.
Rais wa Somalia ameiambia televisheni ya Al Jazeera ya Qatar kwamba: “Utawala wa Kizayuni hauhusiki kivyovyote vile na eneo la Pembe ya Afrika na ni ujuba mkubwa kuiona inatangaza inaitambua Somaliland. Tunashangazwa na uingiliaji wake usio wa lazima.”
Akizungumzia kulaaniwa kimataifa hatua ya Israel ya kuitambua rasmi Somaliland, Rais Sheikh Mahmoud amesema: “Utawala wa Kizayuni umechukua hatua hiyo tulipokuwa tumekaribia kutatua matatizo ya muda mrefu ya nchi yetu na kujaribu kuunganisha nchi kwa amani.”