Guehi

Chanzo cha picha, Getty Images

Muda wa kusoma: Dakika 3

Liverpool bado wana nia ya kumsajili beki wa Crystal Palace wa Uingereza Marc Guehi msimu ujao wa joto, lakini kipaumbele chake ni kujiunga na Real Madrid, ambao pia wanamtaka mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 25. (AS – kwa Kihispania)

Winga wa Manchester City na Norway Oscar Bobb huenda akajiunga na Borussia Dortmund kwa mkopo hadi mwisho wa msimu huu, huku Crystal Palace, Bournemouth na Newcastle wakiwa miongoni mwa vilabu vinavyomtaka mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 22. (Mail – usajili unahitajika)

Juventus inavutiwa na kiungo wa kati wa West Ham na Argentina Guido Rodriguez, 31. (Sky kwa Kiitaliano)

Tottenham wanaweza kumsajili kiungo wa Monaco na Ufaransa Maghnes Akliouche mwenye umri wa miaka 23 mwezi Januari. (Mail – usajili unahitajika)

Roma wanataka kusajili beki mpya na wanawafuatilia wachezaji wawili wa Ligi Kuu ya England, akiwemo mchezaji wa Tottenham mwenye umri wa miaka 23 raia wa Romania Radu Dragusin na mlinzi wa Chelsea wa Ufaransa Axel Disasi, 27. (Sky nchini Italia)

Juventus wana matumaini madogo ya kumsajili kiungo wa kati wa Newcastle Italia Sandro Tonali mwezi Januari, lakini wanalenga kuongeza kasi ya kumsaka mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 25 msimu wa joto. (La Gazzetta dello Sport – kwa Kiitaliano)

Manchester City ina uhakika wa kuipiku Manchester United katika mbio za usajili wa kiungo wa kati wa Nottingham Forest wa Uingereza, Elliot Anderson, 23. (Teamtalk)

Fenerbahce wamewasilisha ombi la kumsajili mshambuliaji wa AC Milan na Ufaransa, Christopher Nkunku, 28. (Calciomercato – kwa Kiitaliano)

.

Chanzo cha picha, Getty Images

Real Madrid wameingia kwenye kinyang’anyiro cha kumsajili mlinzi wa Borussia Dortmund Nico Schlotterbeck, 26, huku klabu hiyo ya Bundesliga ikikadiria thamani ya Mjerumani huyo kuwa takriban £60m. (Sport – kwa Kihispania)

Juventus wanafikiria kumrejesha winga wa Liverpool Federico Chiesa mwenye umri wa miaka 28 kutoka Italia. (La Gazzetta dello Sport – kwa Kiitaliano), nje

Beki wa pembeni wa AC Milan Mtaliano Davide Bartesaghi, 20, ni mmoja wa wachezaji wanaofuatiliwa na Arsenal kabla ya usajili la Januari kumalizika. (CaughtOffside)

Matumaini ya Leeds kumsajili kiungo wa kati wa Nottingham Forest James McAtee yamepata pigo, huku mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 23 pia akihusishwa na kuhamia nje ya nchi. (Football Insider)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *