
Serikali za Mali na Burkina Faso zinazoongozwa chini ya utawala wa kijeshi zimeazimia kuwazuia raia wa Marekani kuingia katika nchi zao, ikiwa ni utekelezaji dhidi ya uamuzi kuwazuia raia wao kuingia nchini Marekani.
Mtandao wa BBC Swahili umeripoti kuwa mataifa hayo mawili yametangaza hatua hiyo Jumanne usiku Desemba 30, 2025, yakisema hatua hiyo inaanza mara moja.
Serikali ya Mali inaongozwa na Rais wa mpito Assimi Goïta chini ya ikiwa utawala wa kijeshi na Burkina Faso inaongoza na Kapteni Ibrahim Traore.
Uamuzi wao unatokana na vikwazo vya usafiri vya Marekani vinavyoathiri mataifa kadhaa barani Afrika na Mashariki ya Kati, kuliidhinishwa na Rais Donald Trump.
Wizara ya Mambo ya Nje ya Mali amesema inatekeleza kanuni ya usawa, na kuongeza kuwa raia wa Marekani sasa watakabiliwa na masharti yaleyale ya kuingia nchini Mali yaliyowekwa na Marekani.
Serikali ya Burkina Faso inayoongozwa na Kapteni Ibrahim Traore imesema itaendelea kujitolea kudumisha usawa wa uhuru, na kwamba bado iko wazi kwa ushirikiano na washirika wa kimataifa ambayo maslahi yanalingana.
Mali na Burkina Faso, pamoja na nchi jirani ya Niger, hivi karibuni zilijiondoa katika jumuiya ya kikanda ya Afrika Magharibi Ecowas na kuunda Muungano wa Mataifa ya Sahel.
Mataifa hayo yamejitenga na washirika wa Magharibi na kuimarisha uhusiano na Urusi.
Nchi nyingine za Kiafrika zilizoathiriwa na marufuku iliyotolewa ya hivi karibuni ya Marekani, ni pamoja na Nigeria na Sierra Leone, zimesema zinapanga kujibu kupitia njia za kidiplomasia.
Hatua iliyochukuliwa na Marekani itaanza kutumika kesho Alhamisi Januari 1, 2026.
Mapema mwaka huu, Chad pia ilichukua hatua ya kulipiza kisasi baada ya kujumuishwa katika awamu ya kwanza ya vikwazo, hivyo ikaamua kusitisha utoaji wa viza kwa raia wa Marekani.
Rais Mahamat Idriss Déby Itno amesema hatua hiyo inahusu utu wa taifa, akiongeza kuwa Chad inaweza kukosa utajiri au ushawishi, lakini haitakubali kudhulumiwa.