Bei za samaki katika soko la Ferry, jijini Dar es Salaam, zimepanda katika siku za karibuni kufuatia kupungua kwa shughuli za uvuvi baharini.

Wafanyabiashara wa samaki sokoni hapo wanasema hali hiyo imesababishwa na upepo wa Kasakazi unaovuma katika Bahari ya Hindi msimu huu, hali inayofanya wavuvi wengi kushindwa kwenda baharini au kuvua kwa kiwango cha kawaida.

✍Juliana James
Mhariri | @claud_jm

#AzamTVUpdates

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *