Visa vya unyanyasaji wa kingono dhidi ya watoto viliongezeka kwa kiasi kikubwa, nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo mwaka 2025, kwa mujibu wa ripoti inayoshughulikia masuala ya watoto UNICEF.

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Ripoti ya UNICEF, inaeleza kuwa watoto zaidi ya 35,000 walibwa na wengine kunyanyaswa katika kipindi cha miezi tisa ya kwanza ya mwaka 2025.

Aidha, Shirika hilo linasema, huenda idadi ya visa hivyo ni kubwa, kwa sababu haviripotiwi kwa sababu ya uoga, vitisho lakini pia sababu za kiusalama.

Mkurugenzi Mkuu wa UNICEF, Catherine Russell, amesema wazazi wanaohofia kuripoti visa vya watoto wao kubakwa kwa hofu ya kunyanyapaliwa au hata kushambuliwa na wahusika.

Idadi kubwa ya visa hivyo, vimeripotiwa katika mikoa ya Kivu Kusini, Kaskazini na Ituri, maeneo ambayo yameendelea kukabiliwa na utovu wa usalama, kwa sababu ya uwepo wa makundi ya waasi.

Jiji la Kinshasa na Kasai pia yameorodheshwa kama maeneo ambayo dhuluma hiyo dhidi ya watoto imeripotiwa kwa sababu ya wasishana wengi kutokea kwenye familia masikinii, wanakabiliwa na changamoto ya chakula huku wengine wakiacha shule, hali ambayo imeendelea kuhatarisha maisha yao.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *