#HABARI: Mwanahabari nguli wa Tanzania anayeishi nchini Sweden, Bwana Majjid Mjengwa, amewataka Watanzania kuwa makini na taarifa za upotoshaji zinazochochewa na watu wenye nia ovu katika mitandao ya kijamii, akisema baadhi yao wanapotosha kwa makusudi ukweli kuhusu hali ya sekta ya usafirishaji nchini.
Mjengwa, ambaye ameishi Sweden kwa zaidi ya miaka 15, amesema uzoefu wake wa kutumia treni za umeme katika nchi hiyo unathibitisha kuwa changamoto za usafiri si za Tanzania pekee, bali ni jambo la kawaida hata katika mataifa yaliyoendelea.
Ameeleza kuwa baadhi ya watu wamekuwa wakieneza upotoshaji mitandaoni kwa madai kwamba mataifa hayo hayakabiliwi na changamoto za usafiri, jambo alilolieleza kuwa ni propaganda zenye lengo la kudhoofisha imani ya Watanzania kwa juhudi za Serikali.
Amefafanua kuwa safari ya treni ya umeme kutoka Dar es Salaam hadi Dodoma sasa huchukua takribani saa tatu na nusu pekee, ikilinganishwa na zaidi ya saa kumi kwa barabara.
Powered by #MCHEZOSUPA
JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:
-
Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.
#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
#Follow @itvtz @radioonetanzania